
Kujenga maarifa kwa uchumi wa kidijitali.
Kuelekea Pure Digitalization. Beula Digital inawawezesha watu na jamii kupata maarifa, mtazamo na mafunzo ya vitendo ya kuelewa mabadiliko, kutatua changamoto na kuzalisha thamani katika uchumi wa kidijitali.
Kubadilisha Fikra. Kukuza Wajenzi.
Beula Digital Platform inawasaidia wanaojifunza barani Afrika kuuelewa uchumi wa kidijitali wa sasa, kufikiri kwa kina, kujenga ujuzi wa vitendo na kuzalisha thamani kupitia teknolojia. Elimu yetu inaunganisha maarifa na vitendo.

Dhamira na Dira Yetu
Kuunganisha maarifa, mtazamo na vitendo katika uchumi wa kidijitali.
Dhamira Yetu
Kupunguza pengo la maarifa ya kidijitali na kuwapatia watu mtazamo, maarifa na ujuzi wa vitendo ili kugeuza uelewa kuwa hatua na kuzalisha thamani katika uchumi wa kidijitali.
Dira Yetu
Kuwa miundombinu ya maarifa ya kidijitali Afrika inayowezesha watu na jamii kujenga suluhisho, biashara na ustawi wa kudumu.

Meet Elizabeth Charles Samoja
Founder & CEO, Beula Digital Platform
Kubadilisha fikra. Kukuza wajenzi. Kuzalisha thamani katika uchumi wa kidijitali.
Beula Digital Platform ilianzishwa ili kuwapatia watu Tanzania na Afrika maarifa, mtazamo na ujuzi wa vitendo wa kushiriki katika uchumi wa kidijitali. Kwa elimu inayopatikana kwa urahisi tunasaidia watu kugeuza maarifa kuwa vitendo, kutatua changamoto, kujenga biashara na kuzalisha thamani ya kudumu.
Elewa. Fikiri Upya. Chukua Hatua. Jenga.
Ushiriki wenye maana katika uchumi wa kidijitali unahitaji kuelewa mabadiliko, kubadili mtazamo, vitendo na kujifunza kila siku.
Elewa Mabadiliko
Tambua kinachobadilika, umuhimu wake na athari katika kazi, biashara na jamii yako.
Jenga Mtazamo wa Kujenga
Chunguza mitazamo ya zamani, fikiri kwa kina na tambua fursa za kutatua matatizo halisi.
Geuza Maarifa Kuwa Vitendo
Tumia unachojifunza. Anza kidogo, fanya mazoezi na tumia teknolojia kuleta suluhisho.
Jenga na Kua
Pima maendeleo, jifunze kutokana na uzoefu na boresha kinachofanya kazi ili kuleta thamani ya kudumu.